Afariki kwenye mashindano ya kunywa pombe kali

Afariki kwenye mashindano ya kunywa pombe kali

Hii imetokea huko Nchini Afrika Kusini ambapo Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30, amefariki dunia baada ya kumaliza chupa nzima ya pombe kali ya Jagermeister.

 

Tukio hilo limemkuta kijana huyo  katika mashindano ya kunywa pombe, yaliyofanyika katika Mtaa wa Mashamba, Limpopo nchini Afrika Kusini.

Mkuu wa Polisi wa Limpopo, Motlafela Mojapelo amesema kijana huyo na wenzake walikuwa kwenye mashindano ya kunywa pombe kali, ambapo mshindi aliahidiwa kupewa kiasi cha randi 200 za Afrika Kusini (takribani shilingi 27,000 za Kitanzania).

Hata hivyo alieleza kuwa  marehemu alifanikiwa kumaliza chupa nzima ya pombe hiyo kali, lakini muda mfupi baadaye alianguka na kupoteza fahamu na baadaye kupoteza maisha.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags