Mshtaki wa ASAP Rocky ambaye ni rafiki yake wa zamani ASAP Relli, anaripotiwa kutoa ushahidi siku ya jana Januari 28 kwa kuelezea mashtaka mawili ya unyanyasaji aliofanyiwa Novemba 6, 2021 katika mtaa wa Hollywood Los Angeles, California nchini Marekani.
“Alinielekezea bunduki, namaanisha imekuwa hivyo kila wakati. Ni ngumu sana kuwa na uhusiano na Rocky, anadanganya sana. Nilimwita mtu wa miezi sita maana ilikuwa namuona kila baada ya miezi sita. Alipofika karibu ilikuwa ni uongo tu. Je, tunapaswa kuwa katika jambo hili na ASAP kwa ajili ya nini? kusema kweli, nisingepigana kamwe na Rocky,"alisema Relli
Hata hivyo aliendelea kutoa ushahidi akithibitisha kwamba hakutaka kugombana kabisa na rapa huyo ambaye alikuwa rafiki yake sana hapo zamani.
“Na huo ndio ukweli wa Mungu. Sina sababu ya kupigana naye tuko kwenye tasnia ambayo unapata blackballed kirahisi sana. Nasema ukweli hapa ndio maana, kwenye video, unaona mimi ni mtu wa kushoto. Alinishika kwa mikono miwili. Na kama ningetaka kupigana naye, ningempiga kwa haki,” alisema Relli.
Hata hivyo waendesha mashtaka wanaelezea kuwa siku ya tukio Relli alipanga kukutana na Rocky kwa ajili ya kurekebisha tofauti zao, lakini yalitokea mabishano ambayo yalisababisha Rocky kuchomoa bunduki na kumuelekezea Relli.
Naye Joe Tacopina ambaye ni wakili wa ASAP amesema Relli amemshtaki ASAP katika mahakama ya kiraia kuhusu tukio hilo, kwa lengo la kupiga hela kwani aliomba kulipwa fidia ya dola milioni 30 kutokana na tukio hilo.
Leave a Reply