Angelina Akiri Kuvuta Sigara Pakti Mbili Kwa Siku

Angelina Akiri Kuvuta Sigara Pakti Mbili Kwa Siku

Mwigizaji wa Marekani Angelina Jolie alikiri kwamba alikua akivuta sigara pakiti mbili kwa siku kabla ya kuanza mazoezi ya kujiandaa kwa na filamu ya Tomb Raider.

Wakati wa mahojiano yake kwenye tamasha la Filamu la Santa Barbara, alifunguka jinsi alivyokuwa akivuta sigara kupindukia huku akiweka wazi mkakati aliotumia kuacha tabia hiyo.

“Nilikuwa nikitumia sigara pakti mbili kwa siku, kwa ajili ya Tomb Raider, nilitakiwa kuacha mara moja, kulikuwa na miezi michache ya mazoezi ya kila siku asubuhi, mchana, na jioni. Nilikuwa katika mazoezi na mwili kupata chakula kizuri, maji, na usingizi.

"Na baada ya kumaliza filamu hiyo, nilijitolea kuishi maisha yenye afya bora na kuacha kabisa uvutaji wa sigara kupindukia,” amesema Jolie

Filamu ya Tomb Raider iliachiwa Machi 15, 2001, ambapo Angelina Jolie akicheza kama Lara Croft.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags