AY alivyobeba dhamana ya Shetta,  video ya Kerewa

AY alivyobeba dhamana ya Shetta, video ya Kerewa

Misifa Camp na Darstamina ni barabara iliyomfikisha alipo leo kimuziki, ibarikiwe mikono iliyowalea Pancho Latino, Mona Gangster na Belle 9 ambao ndio walimleta Shetta katika masikio ya wengi kwa ukubwa huo.  

Utampenda Shetta kwa namna anavyojua kuchagua wasanii wa kushirikiana naye kitu kilichozipa ngoma zake umaarufu kwa miaka yote aliyohudumu katika Bongofleva, kila kolabo kwake imo!. Huyu ndiye Shettta;.

Jina la Shetta alipewa na bibi yake tangu akiwa mdogo, maana ya jina hilo ni samaki mjanja kwa lugha ya kabila lao, ila alianza muziki akitumia jina la Dogo Shetta kabla ya kuondoa hiyo "Dogo" kama walivyofanya Aslay na Muuh wa Mabantu.

Utakumbuka wasanii wengine wa Bongofleva waliopewa majina na bibi zao na kuyatumia kwenye muziki ni Shilole na Malaika.

Kwa mara ya kwanza Shetta alirekodi studio kwa Miika Mwamba, wakati huo alikuwa darasa la nne na mtu aliyemsaidia hadi kumudu gharama za kurekodi ni Ali Choki ambaye alijitolea kumsimamia kimuziki.

Shetta alikuwa ni dansa wa Dully Sykes chini ya Misifa Camp lakini alipoanza kuimba ndipo njia yake ikafunguka na wengi kumfahamu kama Rapa.



Ukaribu wao ndio ulipelekea wimbo wake wa pili kufanya vizuri 'Madananda', kufanyika Dhahabu Records yake Dully Sykes ambaye alishirikishwa pia pamoja na Tundaman.

Baada ya kuachia wimbo wake, Nimechokwa (2011) akimshirikisha Belle 9 ambao ndio ulimtoa kimuziki, Shetta alikuwa akifanya show kwa Sh400,000 tu ila baada ya kuachia ngoma 'Mdananda' akapandisha bei hadi Sh1 milioni.

AY ndiye alifanikisha Shetta kufanya video ya wimbo wake, Kerewa (2014) aliomshirikisha Diamond Platnumz kwa Director Godfather wa Afrika Kusini kwa sababu tayari walikuwa wamefanya kazi pamoja hapo awali.

Kwa ujumla Shetta ni msanii wa pili Bongo kufanya video na Godfather, wa kwanza ni AY, Shetta, Diamond, Linah, Rayvanny n.k.

Gharama ya video yote ya Kerewa ilikuwa ni Dola10,000, takribani Sh25 milioni kwa sasa, AY akachukua Dola7,000 (takribani Sh18.8 milioni kwa sasa) kutoka kwa Shetta na kumpatia Godfather, kwa kifupi AY ndiye alibeba dhamana maana Shetta alikuwa hamjui kabisa Godfather.  

Video ambayo Shetta haipendi kabisa ni ya wimbo wake, Wale Wale (2017) kutokana haikutoka vizuri kama ambavyo aliwekeza fedha nyingi, baadhi ya vipande wameshuti Dubai, huku mastaa kama Jacqueline Wolper na Idris Sultan wakitokea.

Tangazo (product placement) linaloonekana katika video ya wimbo 'Kerewa', Shetta alilipwa Dola10,000, Godfather ndiye alimpatia dili hilo ambapo Shetta alitoa Dola3,000 na kumalizia deni la video hiyo na nyingine iliyobaki akagawa na Diamond.



Mdundo wa wimbo wa Shetta, Hatufanani (2018) akiwashirikisha Jux na Mr. Blue, tayari ulikuwa umetumika katika wimbo wa Nandy, Aibu (2018) kutoka katika albamu yake ya kwanza, The African Princess, mdundo huo umetengenzwa na Kimambo.



Hiyo ni sawa na wimbo wa Professor Jay 'Promoter anabeep' akiwa na Mkoloni na ule wa Ngwea 'Napokea Simu' akimshirikisha Dully Sykes, hizi zimetumia mdundo mmoja uliotengenezwa Bongo Records na P-Funk Majani.

Diamond ndiye alimuunganisha Shetta na Kcee wa Nigeria aliyemshirikisha katika wimbo wake, Shikorobo (2015), hadi wanamaliza kurekodi wimbo huo walikuwa hawajaonana, walitumiana tu sauti. Shetta na Kcee walionana kwa mara ya kwanza Afrika Kusini walipoenda kwa ajili ya kushuti video ya wimbo huo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags