Baada Ya Kuachana Na Manara, Zaiylissa Afunguka Kwa Mara Ya Kwanza

Baada Ya Kuachana Na Manara, Zaiylissa Afunguka Kwa Mara Ya Kwanza

Aliyekuwa mke wa Haji Manara, Zaiylissa amefunguka kwa mara ya kwanza huku akiweka wazi kwasasa hayupo kwenye ndoa na ameamua kupumzika kwanza.

Zai ameyasema hayo mapema leo Aprili 12, 2025 mbele ya waandishi wa habari huku akiweka wazi zaidi kuhusiana na Manara kutohusika kabisa kwenye mikataba yake.

“Sipo kwenye ndoa kwasasa na napumzika kwanza. Kuhusu mkataba wa kwanza, press ya kwanza tulikuwa na aliyekuwa mume wangu nilitafutwa kabla mimi sijakutana na aliyekuwa mume wangu kwahiyo nilitafutwa na tukakubaliana kufanya kazi.

"Bahati nzuri likatokea la kutokea mambo yakaunganika tukaendelea na kazi humo humo moja kwa moja na kuhusu yeye alikuwa hanisainii kwenye mikataba yangu, alikuwa ananisaidia na kunisimamia kama mke wake, mikataba nasaini mwenyewe, alikuwa ananisapoti si kwamba alikuwa kwenye mikataba,” amesema Zaiylissa.

Aidha ameweka wazi kuhusiana na baadhi ya tetesi zinazoeleza kuwa ana mpango wa kurudi kwa mpenzi wake wa zamani, Dullah Makabila ambapo ameeleza hana mpango wa kurudi kwa yeyote.

“Hizo video ni za muda mrefu sana halafu sina mpango huo wa kurudi kwa yeyote, sasa hivi nimeamu kuforcus na kazi, familia, yaani sasa hivi vitu mtakavyoviona kwangu mimi ni kazi basi,” amesema mwigizaji huyo wa Tamthilia ya Juakali na kuongeza.

“Lakini niwaambie tu ndoa sio mbaya, na wasikurupuke pia, kila kitu kinakuja kwa wakati sahihi na mtu sahihi anakuja wakati sahihi, yaani hivyo tu wasikurupuke.”

Utakumbuka kuwa siku mbili zilizopita Haji Manara na Zaiylissa waliingia katika ugomvi mkubwa uliopelekea kurushiana maneno katika mitandao ya kijamii wakionesha kuwa penzi lao limefika mwisho.

Wawili hao walifunga ndoa Januari 24, 2024 huku ikiwa ni ndoa ya sita kwa Manara na ya pili kwa Zaiylissa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags