Imeripotiwa kuwa hali si shwari kwa wanamuziki kutoka Marekani Kanye West na Taylor Swift baada ya timu ya Swift kudaiwa kuwa na mpango wa kumshitaki Ye.
Hivi karibuni, Taylor alitoa wimbo wa ‘thanK you aIMee’ katika albamu yake mpya ya ‘The Tortured Poets Department’ ambao mashabiki wanaamini kuwa wimbo huo ulikuwa unamlenga Kanye kutokana na herufi kubwa katika kichwa cha wimbo zinazoweza kuunda jina la ‘Ye’.
Aidha kufuatia na hilo Kanye hakulikalia kimya aliingia katika mitandao ya kijamii akitoa lugha za matusi huku akimlalamikia Taylor alihusika katika kumzuia kutumbuiza kwenye hafla ya Super Bowl miaka ya nyuma.
Moja ya jumbe za Kanye ambazo zimezua mjadala katika mitandao ya kijamii ni kumzalilisha Swift kwa kuandika kuwa aliwahi kulala na Justin Beiber pamoja na Harry Styles kwa wakati mmoja.
Kutokana na matusi hayo timu ya Taylor imeiandikia barua kampuni ya X kufuta haraka jumbe za Kanye kwani zainamzalilisha Swift huku kukiwa na tetesi kuwa msanii huyo anajiandaa kumfungulia mashitaka Ye.
Taylor na Kanye wamekuwa kwenye ugomvi mkubwa kwa zaidi ya miaka 10 ugomvi ambao ulianza mwaka 2009 wakati wa ugawaji wa tuzo za Tuzo za MTV Video Music Awards, ambapo Kanye alikatiza hotuba ya ushindi ya Taylor kwa kusema kuwa Beyoncé alistahili tuzo hiyo.

Leave a Reply