Beyonce Hufanya Tambiko Hili Kila Mwisho Wa Mwaka
Nyota wa muziki kutoka Marekani, Beyonce ameweka wazi utaratibu wake wakufanya tambiko kila anapomaliza mwaka ambapo hulifanya kwa kujirusha katika bahari.
Imeripotiwa kuwa Beyonce na Jay Z husafiri hadi St. Barths na kutumia muda wao kwenye boti binafsi ya kifahari 'Yachty' kusherehekea mwaka mpya na huwa anafanya tambiko hilo kwa kuruka ndani ya maji huku akiamini kuwa huyaacha mambo yaliyotokea mwaka uliopita na kuanza mwaka mpya akiwa safi.
“Sijui nina shida gani, Nilitazama picha na kusema, Huo ni ujinga kweli. Ninafanya kila mwaka, kuruka kwangu hiyo ni ibada. Hiyo ni kuacha kwangu mambo yaliyotokea mwaka uliopita na kuanza upya, hii ni likizo na niko huru.
Lazima niruke kitu ili niweze kuacha kila kitu kilichotokea kabla ya likizo iliyopita. na kuanza upya Ni kama nimebatizwa,” Beyonce aliimbia Rolling Stone.
Leave a Reply