Rais wa Marekani Joel Biden ametangaza nia yake leo Aprili 25, 2023 licha ya utafiti uliofanywa na Kituo cha Runinga cha NBC kuonesha 70% ya wananchi hawataki rais huyo agombee tena Urais.
“Nilipogombea urais miaka minne iliyopita, nilisema tuko kwenye vita vya kuipigania Marekani na bado tuko” Biden alisema katika video ya dakika 3 akitangaza kugombea kwake.
Akiwa na umri wa miaka 80, Biden ndiye rais mwenye umri mkubwa zaidi kuhudumu katika kiti cha urais nchini Marekani.
Aidha mwishoni mwa wiki vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kwamba Joe amemchagua mshauri wake mkuu wa White House ni Julie Chavez Rodriguez kama meneja wake wa kampeni.
Katika taarifa hiyo iliyoambatana na video ya uzinduzi ulio fanyika siku ya Jumanne Biden alithibitisha kuchaguliwa kwa Rodriguez, mshirika wa muda mrefu wa Latina Democratic na uhusiano na Rais wa zamani Barack Obama na Makamu wa Rais Kamala Harris.
Leave a Reply