Baada ya bondia wa ngumi za kulipwa, Floyd Mayweather kumwagia sifa Rais wa Marekani Donald Trump kuwa ni Rais bora, sasa mwanamuziki 50 Cent hakulikalia kimya suala hilo huku akimjibu kwa mafumbo bondia huyo.
Kupitia ukurasa wake wa X (zamani twitter) 50 ametuma fumbo hilo kwa Mayweather akidai kuwa sifa hizo ni kama za mtoto anayekula kalamu darasani.
“Unajua pale unapokuwa shuleni na mtoto anatafuna kalamu sasa unaona nini kinatokea wanapokuwa wakubwa, kabisa unasema kuwa ni Rais Bora,” ameandika 50
Mayweather wakati alipokuwa kwenye mahojiano na ‘Fox Business’, alimwagia sifa Rais Trump akidai kuwa ndiye Rais bora kuwahi kutokea katika historia ya Marekani jambo ambalo 50 Cent hakubaliani nalo kabisa.
Ikumbukwe wawili hao waliwahi kuripotiwa kuwa na ugomvi mwaka 2012 kuhusiana na masuala ya maokoto lakini miaka ya hivi karibuni walidaiwa kumaliza tofauti zao.

Leave a Reply