Kupitia instastory ya msanii huyo ameweka wazi kuwa tayari ameshatinga nchini hapo kwa ajili ya show hiyo huku akiweka wazi kuwa atadili na watakaofanya vurugu.

“Nairobi, niko hapa! Heshima na upendo nilio nao kwa Burna Boy ni mkubwa sana. Twendeni tukapige shangwe kesho, nimeshanunua tiketi zangu! Tutaonana huko, nataka kumuona akichana na kuimba.
Imepita muda mrefu tangu nimuone brosk wangu. Na kwa msanii yeyote atakayejifanya analeta vurugu, jueni niko karibu! Muulizeni Eric Omondi, anajua jina hili,”ameandika Konde Boy
African Giant anatarajia kukiwasha nchini Kenya, Machi Mosi, 2025 Uhuru Gardens, kupitia tamasha la ‘MadfunXperience’ litakalo mkutanisha na wasanii wengine kama Vigro Deep, Charisma, Bensoul na wengineo.
Leave a Reply