Ben Pol: Nikiacha Muziki Sitotangaza

Ben Pol: Nikiacha Muziki Sitotangaza

Msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa ikitokea kaamua kuacha muziki hakutakuwa na tangazo wala waraka.

“Japo sijafikiria na sina mpango huo kabisa! lakini ikitokea siku nikaamua kuacha kufanya Muziki hakutakuwa na tangazo, wala waraka…kama ambavyo miaka kadhaa nyuma watu walishtukia tu kuna mtu anaitwa Ben Pol anaimba, vivyo hivyo watashtukia kuna mtu alikuwa anaitwa Ben Pol ila siku hizi haimbi.

Moyoni nitakuwa na amani kwamba nimehudumu vizuri kwa nyimbo, maisha yangu na jumbe villivyogusa maisha ya watu na ku-inspire, kwa sababu ni Kweli, na hilo nikijua mimi itakuwa imetosha, mengineyo yatakuwa ni ziada,” ameandika Ben Pol.

Amesema haamini katika kuacha alama kwakile alichofanya kwa sababu ni mambo ya kutaka kujipa umuhimu baada ya kuondoka.

“Binafsi siamini sana kwenye ‘Legacy’ naona ni mambo ya kutaka kujipa umuhimu hata ukishaenda, Naona ni kitu kilianzishwa zamani na Mtawala, Mfalme au Mtu mwenye nguvu ambaye hakuwa humble.. wazo lake lilikuwa kwamba hata akienda aendelee kuheshimiwa, kusujudiwa au kutajwa kwa yale aliyoyafanya, Sidhani kama ina tija!

Maisha ya binadamu yameanza zaidi ya miaka 200,000 iliyopita, kweli kabisa tukukumbuke?! Sasa tutakumbuka watu wangapi? Au kwamba miaka 200,000+ ijayo wanadamu wa wakati huo watukumbuke sisi wa sasa?, ni kazi ngumu sana kuwapa waja katikati ya mambo yote yanayoendelea Duniani; Climate change, Umasikini, Kukosekana kwa usawa wa Vipato, Afya, Chakula na Maji , Haki za Binadamu, Silaha za Nyuklia, AI n.k,”ameandika Ben Pol






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags