Hali ya Mushizo bado, moshi waingia kwenye kifua

Hali ya Mushizo bado, moshi waingia kwenye kifua

Hali ya mwanamuziki wa Singeli Mussa Ramadhan maarufu ‘Dj Mushizo’ inaendelea kuimarika ikiwa ni takribani wiki tatu tangu apate ajali ya moto na kufikishwa katika Hospitali ya Rufaa Amana kwa ajili ya matibabu.

Akizungumza na Mwananchi meneja mkuu wa msanii huyo Mkumbange ameeleza kuwa kwa sasa Mushizo anaendelea na matibabu huku sababu inayoendelea kumweka hospitalini hapo ni maumivu ya kifua yaliyosababishwa na moshi aliovuta wakati wa moto.

“Mgonjwa sasa hivi anaendelea vizuri kidogo lakini kinachomsumbua sana sana sasa hivi ni kifua kwa hiyo hata akiongea hivi anaongea kwa shida. Kwa sasa anatumia dawa wanasema ni moshi uliingia kwa wingi.

Niliongea naye jana kumuuliza kama walishampiga ex-rey akaniambia bado lakini wanasema uliingia sana na akitumia dawa atakaa sawa. Bado hajaruhusiwa yupo Amana, kuhusu vidonda kidogo afadhali kwa sababu walimchuna na mashine ili dawa iweze kupita vizuri,” amesema Mkumbange.

Aidha aliongezea kwa kueleza “Japo vidonda havijapona lakini anaendelea vizuri inatia moyo kwa kiasi chake ni hicho kifua tu ndio kinambana sana, kuhusu kuruhusiwa madaktari bado hawajatoa taarifa rasmi watamruhusu lini kwa sababu anaendelea na matibabu kila siku wanamchoma sindano nyingi, madawa mengi kwa hiyo bado hawajatuambia lini atatoka,”amesema Mkumbange

Mushizo alipata ajali ya moto nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam majira ya 12 jioni, Juni 12, 2025 huku chanzo cha moto kikitajwa kuwa ni shoti ya umeme.

Nyimbo zilizompa umaarufu Mushizo ni Wivu pamoja na Mapenzi Hisia, ambazo zinafanya vizuri kwa sasa katika mitandao ya kuzikiliza muziki kama YouTube.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags