Kolabo Ya Rayvanny Na Maluma Ilikuwa Hivi

Kolabo Ya Rayvanny Na Maluma Ilikuwa Hivi

Mkali wa Bongo Fleva ambaye ameendelea kuupeleka muziki huo Kimataifa Rayvanny amefichua alivyofanikiwa kumshawishi Maluma kufanya naye kolabo ya wimbo wa ‘Mama Tetema’.

Baada ya kumuona Maluma kwenye tukio la ‘Fashion Week’ huko Los Angeles, akifurahia moja wimbo wake ndipo alipoamua kuzama DM yake ya Instagram ambapo msanii huyo hakumjibu chochote.

“Nilimtumia ujumbe, ‘Bro, asante kwa kufurahia wimbo wangu. Natamani tufanye kitu pamoja.’ Lakini hakujibu kwa siku kama nne,” amesema Vanny Boy

Aidha baada ya ukimya huo Chui alidai kuwa aliamua kuchukua uamuzi wa kuposti picha yake na Maluma na kuandika kuna kitu kikubwa kinakuja, na mara baada ya picha kutrendi katika mitandao ya kijamii ndipo Maluma alijibu DM zake.

“Niliposti picha yangu na Maluma na kuandika something coming. Alipoona tukio hilo limepewa attention kwenye mitandao na blogu alinitumia DM na kusema, Tufanye remix ya wimbo huo. Kutoka hapo, kila kitu kikaendelea vyema,” alisema Rayvanny

Wimbo "Mama Tetema" wa Maluma akimshirikisha Rayvanny uliachiwa rasmi mwaka 2021, huku ukitazamwa zaidi ya mara milioni 54 kupitia mtandao wa YouTube. Wawili hao walifanya show ya kwanza ya wimbo huo kwenye tuzo za MTV EMA mwaka 2021.

Mwaka 2022, wimbo huu ulitunukiwa Tuzo ya African Entertainment Awards, USA (AEAUSA) katika kipengele cha Kolabo Bora ya Mwaka. Pia, "Mama Tetema" ilijumuishwa katika albamu ya Maluma iitwayo "Don Juan", ambayo ilipendekezwa kuwania Tuzo za Grammy za mwaka 2024.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags