Kumbe ile suti Dully Sykes aliazima kwa Joseph Kusaga

Kumbe ile suti Dully Sykes aliazima kwa Joseph Kusaga

Kwa miaka zaidi ya 25, Dully Sykes amekuwepo katika muziki akifanya vizuri kwa nyimbo zake maarufu huku akitoa albamu tatu ambazo ni Historia ya Kweli (2002), Handsome (2004) na Hunifahamu (2005) zilizomtangaza vizuri.

Ukiachana na kuimba, Dully Sykes ana mchango mkubwa wa kuikuza Bongofleva kwa kuwasaidia wasanii wengi ambao sasa baadhi yao wana majina makubwa huku akianzisha studio ambayo alitoa mikwaju ya maana kabisa. Fahamu zaidi.

Kwa mujibu wa Dully Sykes, yeye ndiye mwanzilishi wa Bongofleva kwa kuja na mtindo wa kuimba kupitia wimbo wake ‘Julieta’ baada ya wasanii wengi hapo awali kufanya rap, huku akimtaja Alikiba kutokea Kings Music kama mfalme wa Bongofleva.

Anamtaja Alikiba kama mfalme wa Bongofleva kwa sababu ndiye msanii wa kwanza ambaye alikuwa bado hajatoka kimuziki, lakini akamuomba amshirikishe katika wimbo wakati tayari yeye alikuwa msanii mkubwa, kipaji cha Kiba ndicho kilichomvutia.

Kipindi Lady Jaydee anafanya kazi Clouds FM, ndiye alikuwa mtangazaji wa kwanza kuucheza wimbo wa Dully Sykes ‘Julieta’ redioni, ni wimbo uliobadilisha maisha ya Dully ni ndio unatajwa kama wa kwanza wa Bongofleva.


Aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi, Clouds Media Group, hayati Ruge Mutahaba alipousikia tu wimbo wa ‘Julieta’ alivutiwa nao na kumpa Dully Sykes fedha kiasi cha Sh10,000 akanunue viatu maana hakuwa navyo wakati huo.

INSHU YA SUTI ILIKUWA HIVI

Suti aliyovaa Dully Sykes katika cover ya albamu yake ya pili, Handsome (2004), aliazima kwa Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga, hivyo baada ya kumaliza kupiga picha akarudisha suti ya Kusaga.

Kusaga aliamini sana katika kipaji cha Dully. Aliamini albamu hiyo itafanya vizuri sokoni pindi itakapotoka, basi akamuazima suti yake na kweli albamu hiyo aliyoizindua akiwa na TID ikawa na mafanikio zaidi ya ile ya mwanzo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags