Rais Joe Biden ampa medali ya heshima denzel washington

Rais Joe Biden ampa medali ya heshima denzel washington

Rais Joe Biden amemtunuku mwigizaji Denzel Washington heshima ya juu kabisa ya uraia kwa medali ya Uhuru wa chini hapo jana katika Ikulu ya White House nhini Marekani.

Medali hiyo ambayo imetolewa na Rais Joe Biden Ikulu ya White House ikiwa ni heshima ya juu zaidi ya kiraia nchini Marekana inayotolewa kwa watu ambao wametoa michango ya mfano kwa ustawi wa maadili, usalama wa amani ya ulimwengu, Juhudi zingine muhimu za kijamii au za kibinafsi.

Utakumbuka mwigizaji huyo mwezi uliopita alitaangaza kustaafu kuigiza huku akiweka wazi kuwa Black Panther 3 Gladiator 2, na Othello zitakuwa zake filamu zake za mwisho kucheza.

Kwa miaka zaidi ya thelathini Denzel amekuwa na ushawishi mkubwa katika tasnia ya filamu, akifanya kazi kama mwigizaji, muongozaji, na mtayarishaji wa filamu huku akionesha umahiri wake waakucheza uhusika mbalimbali kuanzia uhusika wa kihistoria hadi wa kisasa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags