Leornado Atamba baada ya kushinda tuzo Mchekeshaji bora wa mwaka

Leornado Atamba baada ya kushinda tuzo Mchekeshaji bora wa mwaka

LEORNADO ATAMBA BAADA YA KUSHINDA TUZO

Baada ya mchekeshaji Leornado kushinda tuzo ya 'Overall Best Comedian of the year' kupitia tuzo za Tanzania Comedy Award, ambazo zilitolewa jana Februari 22, 2025. Kwenye ukumbi wa The Super Dome Masaki. Mchekeshaji huyo ameeleza furaha yake na kuahidi kuendelea kufanya makubwa zaidi kwenye tasnia ya uchekeshaji.

"Kiukweli tuzo yangu nimeipokea kwa ukubwa kwa sababu ndio tuzo ambayo Overall kati ya wengi. Mimi ndio mkubwa wao kwahiyo namshukuru Mungu sana nashukuru mashabiki kwa sababu walikuwa wananipambania sana," amesema Leonardo.

Leonardo ambaye alikuwa akiwania vipengele vitatu kwenye tuzo za Tanzania Comedy Award, ameongezea kuwa amefarijika sana kushinda kipengele hicho kimoja ambacho ni kikubwa kwa tuzo hizo.

"Kichwani nilikuwa nawaza kama nisipopata zile mbili basi nipate hii moja kubwa kwahiyo nilivyoona nimekosa mbili zile nikasema Eeh! sasa imebiki ile moja kubwa. Lakini nashukuru Mungu nimepata Moyo umesuuzika kwa kweli," amesema Leonardo.

Hata hivyo, licha ya tuzo hizo kuwa na maneno mengi baada ya kutambulishwa kwake mapema mwaka 2025. Kwa upande wake Leornado amesema haki imetendeka na kila aliyechukua tuzo alistahili.

"Nadhani kila sehemu ambayo imeenda tuzo ni sahihi kwa sababu ukiangali wachekeshaji wengi wamekuwa na muendelezo mzuri wa kufanya kazi za ucheshi. Kwa mwaka mzima kwahiyo ukiangalia unaona kabisa kila aliyechukua amestahili,"amesema Leonardo.

Leornado amezungumzia kumbukumbu yake nzuri aliyoipata usiku huo wa tuzo za wachekeshaji nchini ambazo mgeni rasmi alikuwa Rais Samia Suluhu Hassan na kuhudhuriwa na viongozi wa Basata na Bodi ya Filamu.

"Nadhani ule muda wa maokoto lakini kwanza kufanya tu ucheshi mbele ya Rais ni kitu kikubwa sana. Kwa sababu ametupa muda wake kutusikiliza mawazo yetu lakini matukio yote ni mengi,"

Ushindi wa tuzo hiyo ya Best Comedian Of The Year Overall umemfanya Leornado kukabidhiwa Sh 30 Milion kutoka kwa waandaji wa tuzo hizo chini ya mmiliki wa mchongo huo Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' lakini pia kwa kila mchekeshaji aliyepafomu mbele ya Rais alipata bahasha ya fedha.

"Nimechukua usiwaambie watu namshukuru sana Rais japo sijahesabu lakini najua ni nyingi uzito wake ni kuanzia milioni na kuendelea, amesema Leonardo,"






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags