Mashabiki Wa Fally Ipupa Wamvaa Asake

Mashabiki Wa Fally Ipupa Wamvaa Asake

Mkali wa Afrobeats kutoka Nigeria Asake, amejikuta katikati ya utata na mashabiki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambao wametishia kumfungia msanii huyo kufanya matamasha na kuingia nchini humo kisa Fally Ipupa.

Asake amejikuta katika sakata hilo baada ya mfalme wa muziki Congo Fally Ipupa, kudai alimtafuta msanii huyo kwa ajili kufanya naye kolabo lakini Asake alimpatia majibu yasiyofaa.

Inaelezwa kuwa Fally alikuwa akijiandaa kutoa album yake na kuwa alitaka Asake aweke mistari yake kupitia moja ya wimbo wake. Lakini Asake aliomba kiasi kikubwa cha fedha ili aweze kufanya naye kolabo ambapo alitaka zaidi ya dola 7,000 ikiwa ni Sh 16 milioni.

Hata hivyo Fally alishangazwa na ombi na kiasi hicho kikubwa cha fedha ambacho kilimfanya aone kudharauliwa na msanii huyo ambaye siku mbili zilizopita alishutumiwa kwa kutomsaidia baba yake mzazi ambaye ni mgonjwa.

Kupitia mitandao ya kijamii mashabiki wamezua mijadala mbalimbali huku wakieleza ombi hilo la Asake ni kama dhihaka kwa msanii wao ambaye amekuwa akifanya vizuri na kutambulika kimataifa.

Hata hivyo, licha ya mvutano huo, utakumbuka Fally na Asake waliwahi kutoa remix ya wimbo wa "Sungba", ambao ulifanya vizuri katika nchi mbalimbali.

Fally Ipupa ni mmoja wa wasanii wanaohusishwa kuutangaza muziki wa rumba na soukous kimataifa kupitia ngoma zake kama "Eloko Oyo,'Original,' na 'Sexy Dance' zikipata umaarufu mkubwa na kujizolea mashabiki kila kona.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags