Baada ya kumalizika kwa sherehe ya Hamisa Mobetto na Aziz Ki, sasa mashabiki wamehamia upande wa Paula Paul na Marioo wakiwataka wawili hao waoane.
Kupitia mitandao ya kijamii, zinasambaa picha za wawili hao wakiwa pamoja. Huku mashabiki wakitoa maoni kutaka Marioo afunge ndoa na Paula kabla hajachelewa.
“Oa huyo mtoto Marioo usituletee masihara”, “Mnapendeza sana mashallah Paula she’s taking good care of Marioo, my Favourite Tanzanian couple”, “Oa tu jamani na sisi mashabiki zenu tufurahi,” huku mwingine akiandika “Marioo muoe Paula bwana She deserve it”.
Uhusiano wa wawili hao ulianza baada ya Paula kutemana na msanii Rayvanny mwaka 2022. Tangu kuwa pamoja wawili hao wamekuwa wakionekana katika mitandao ya kijamii wakiwa na furaha, amani, ushirikiano na upendo. Hivyo basi mashabiki wanaamini kuwa wawili hao watakapofunga ndoa watakuwa wametimiza ile kauli ya ‘Couple Goals’.
Mbali ya kupata mtoto pamoja aitwaye Amarah, lakini mashabiki wanabariki wawili hao kuoana kwa sababu wanaendana na wanastahili kuwa pamoja “Nyie wawili mnaendana sana msijaribu kuja kuachana”.
“Marioo utaua sana ukimuoa Paula yaani nyie wawili mnapendezana sana embu fanya kweli uwazibe midomo wambea”, huku mwingine akimwaga sifa zaidi “Twende mbele turudi nyuma hawa watu wawili wanapendana sana, waoane tuu maana wanaendana kwenye kila kitu wote saizi sawa,”
Utakumbuka tetesi za uhusiano wa Marioo na Paula zilianzia Aprili 2023, baada ya mrembo huyo kuachana na Rayvanny, tangu wakati huo wamekuwa pamoja. Ukiwa ni uhusiano wa kwanza wa Marioo kuuweka hadharani tangu kuhusishwa na Mimi Mars.
Uhusiano wa wawili hao umekuwa wa faida kwa mara kadhaa huku Marioo akimtumia Paula kama video Queen kwenye ngoma kadhaa kama ni Lonely (2023), Tomorrow (2023) na Sing (2023).

Hata hivyo, mwishoni mwa 2024 Marioo alisema mipango ya kumuoa Paula tayari imefanyika hivyo siku yoyote atatangaza tarehe ya ndoa.
"Sisi tupo kama familia suala la ndoa ni dogo sana, ni kuamua na sheria tumeanza kufuata, mambo ya msingi tumeshafanya imebakia suala la kusema tarehe fulani tunataka kuoana, mpango huo upo kwa sababu nampenda, amenizalia mtoto mzuri kwa hiyo kama hitaji lake ni ndoa ni dogo sana barua tulishapeleka," alisema Marioo.
Leave a Reply