Mwigizaji wa Coming to America afariki dunia

Mwigizaji wa Coming to America afariki dunia

Mwigizaji wa Marekani John Amos ambaye alipata umaarufu kupitia filamu ya ‘Coming to America’ na ‘Good Time’ amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84.

Taarifa ya kifo chake imetolewa na mtoto wake Kelly Christopher Amos akieleza kuwa baba yake alifariki Agosti 21, mwaka huu lakini waliamua kutotoa taarifa ili waweze kupata muda wa faragha na familia huku sababu ya kifo chake haikuwekwa wazi.

Kabla ya kuanza kuonekana kwenye filamu, Amos alicheza soka katika Chuo Kikuu cha Colorado State na alikuwa mchezaji wa muda mfupi wa Kansas City Chiefs.

Alianza kuonekana kwenye filamu mwaka 1974, katika filamu ya ‘Good Times’ ambapo alicheza kama baba mwenye ujasiri aliyepewa jina la James Evans.

Enzi za uhai wake ameonekana kwenye filamu kama ‘Roots’ akiwa kama Kunta Kinte, Coming to America, Die Hard 2, The West Wing, Block Party, Bad Ass 3: Bad Asses on the Bayou na nyinginezo nyingi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags