Tegemea uhusika wa Paul Walker kwenye 'Fast & Furious

Tegemea uhusika wa Paul Walker kwenye 'Fast & Furious

Mwigizaji na mtayarishaji wa filamu nchini Marekani, Vin Diesel amethibitisha kuwa Uhusika wa marehemu Paul Walker, anayejulikana kwa jina la Brian O’Conner katika mfululizo wa filamu za Fast & Furious, unarejea katika filamu hiyo.

Akizungumza mbele ya umati wa mashabiki kwenye Fuel Festival huko California, Juni 28, 2025, Diesel akiwa ameungana na waigizaji wengine wa "Fast and Furious" ambao ni Tyrese Gibson na Cody Walker alithibitisha hilo.

Wakati wa mwonekano wake wa muda mfupi, Diesel aliuambia umati huo wa mashabiki watarajie kuona uhusika wa Paul Walker kwenye filamu ya mwisho ya 'Fast and Furious' inayotarajiwa kutoka Aprili 2027 kwani ameiomba timu yake ya uzalishaji.

"Studio iliniambia, 'Vin, tafadhali tunaweza kuwa na fainali ya 'Fast and Furious' Aprili 2027? Nilisema, 'ndio lakini Chini ya masharti matatu.' Kwanza, ni kurudisha franchise L.A.!Jambo la pili lilikuwa ni kurudi kwenye utamaduni wa magari, kwenye mbio za barabarani! Jambo la tatu lilikuwa kuwaunganisha tena Dom na Brian O'Conner." amesema.

Paul Walker alifariki akiwa na umri wa miaka 40 mwaka 2013 baada ya kupata ajali ya gari, ikiwa ataigiza kwenye sehemu ya mwisho ya "Fast and Furious," itatumika teknolojia 9AI) kuupata uhusika wake.

Filamu yao ya mwisho ya 'Fast X,' ilitolewa Mei 2023, ilifanikiwa kuingiza zaidi ya dola 700 milioni duniani kote wakati iligharimu zaidi ya dola 340 milioni kufanikisha uzalishwaji wake kukamilika

Miongoni mwa waigizaji waliyocheza humo ndani ni pamoja na Vin Diesel, Alan Ritchson, Jason Momoa, Michelle Rodriguez, Rita Moreno na Brie Larson.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags