Ne-Yo Awatambulisha Wapenzi Wake Wanne

Ne-Yo Awatambulisha Wapenzi Wake Wanne

Msanii wa R&B kutokea Marekani, Shaffer Chimere Smith maarufu kama Ne-Yo amethibitisha kuwa yuko kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanawake wengi akiwatambulisha wanawake zake wanne kwa mashabiki.

Mkali huyo kupitia post yake aliyoweka Instagram jana Machi 10, 2025, aliwatambulisha wanawake wanne ambao ana uhusiano nao kwa sasa.

Aliweka wazi kuwa yeye na wanawake hao wanne wote wanafuraha katika uhusiano huo, huku akiwataka watu ambao wanakosoa uamuzi wake kuendelea na maisha yao.

"Kwa kuwa ulimwengu unavutiwa sana, nadhani ninapaswa kuwatambulisha wapenzi wangu ipasavyo. Mabibi na mabwana, ninawasilisha wapenzi wangu" amesema Ne-Yo akiwatambusha wapenzi wake ambao ni Cristina, Arielle, Moneii, na Bri.

Ne-Yo alisisitiza kuwa mamuzi yake hayo yanatokana na uwazi akisema kuwa anahakikisha kila mwanamke aliyenaye kwenye mahusiano hayo anamfahamu mwenziye "Ninakupenda wewe, lakini pia ninampenda huyu, yule na yule"

Hapo awali, Ne-Yo alifunga ndoa na mtangazaji wa Tv Crystal Renay Smith kabla ya kutengana kwao mwaka 2023, kwa ripoti ya jarida la People inasema kuwa Crystal alimshitaki Ne-Yo kwa kuwa na mtoto na mwanamke mwingine wakati wa ndoa yao. Wawili hao walibarikiwa kupata watoto watatu pamoja.

Lakini Pia, Neyo ana watoto wawili na mtangazaji 'Monyetta Shaw-Carter' na watoto wengine wawili alipata na mshawishi Sade Jenea Bagnerise ambaye Aprili, 2024 alimshitaki msanii huyo kwa kutelekeza watoto na kumshambulia kimwili mpaka kufikia hatua ya kumuita Ne-Yo 'Diddy Jr'.

"Waambie kuhusu kituko Diddy mdogo unajua ulichofanya. Ulinipiga mwili sakafuni. Waambie wewe halisi na kwa nini tuko hapa leo?" Alisema mwanamke huyo huku akihoji kwanini Ne Yo hataki kutulia na watoto nyumbani.

Hata hivyo, mwaka jana Bagnerise alizungumza hadharani kuhusu uhusiano wake na mzazi mwenza Ne-Yo, ambaye anadai ana uraibu wa ngono.

"Ninaendelea kusikia na kuona pande zote tofauti kuhusiana na tabia yake nimeona mambo mawili. Kila mtu ikiwa ni pamoja na mama yake, washirika, mimi, na Crystal wote wamesema na kukubaliana kwamba hakuna hata mmoja wetu anayeweza kumtambua mtu huyu ambaye amekuwa,"aliandika Bagnerise






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags