Diamond Aendelea Kukimbiza Boomplay

Diamond Aendelea Kukimbiza Boomplay

Mwanamuziki Diamond Platnumz ametajwa kuwa msanii wa kwanza Afrika Mashariki na Kusini kufikisha stream milioni 500 kwenye mtandao wa kusikiliza na kuuza muziki Boomplay.

Rekodi hiyo ni ishara nzuri ya mafanikio kwa msanii huyo, ambayo imetokana na juhudu, ubunifu na kuchukulia muziki kama kazi jambo ambalo linamfanya atambulike kimataifa.



Msanii huyo anakuwa kinara na kuwapiku mastaa mbalimbali ndani na nje ya Tanzania akiwemo Yemi Alade mwenye stream 400 milioni, Alikiba stream 200, Sauti Sol mwenye zaidi ya stream 200 huku vinara Afrika wakiwa ni Burna Boy, Wizkid na Davido wenye zaidi ya stream 1 bilioni.

Mastaa wengine kutoka Tanzania wenye wasikilizaji wengi ni pamoja na Zuchu 370, Harmonize 373, Jay Melody 340, Rayvanny 340, Mbosso 325, Marioo 280, Alikiba 200, Nandy 146 na Juz ambaye ana wasikilizaji 123 milioni.

Mbali na kupata mafanikio hayo wiki hii. Pia msanii huyo alishinda Tuzo za Trace 2025 katika kipengele cha Msanii Bora wa Kimataifa. Akashinda tena kipengele hizo kwenye Tuzo za Galaxy Music Awards zilizotolewa nchini Senegal, katika mji mkuu wa Dakar.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags