Njaanuari Na Huba La Pisi Kali Kwa Vizee

Njaanuari Na Huba La Pisi Kali Kwa Vizee

Unakatiza zako kitaa. Iwe Mlimani City ama Sinzani kwenye maduka yao yale ya shumizi na vijora. Mara paap unakutana na karembo flan hivi amazing. Unaona kukaacha kapite hivi hivi, utakuwa ubwege

Unakapa 'hai' sambamba na sifa za uongo. Jitahidi ziwe sifa feki maana ukikapa za ukweli ni dhambi. Hivi vitoto vya 2000 vinapenda kupigwa kamba sana. Havilali bila kupigwa fiksi 1000 kwa siku na vinakubali.

Kinakuuliza: ''Una miaka mingapi?'' unajibu: "32." Utasikia: ''Oh my gosh, we mdogo, mi 'nameki lavu' na 'fote faivu abavu,' 'kozi' wanajua kupenda na wanajali, nyie vijana wasumbufu, kwa kweli siwawezi. Amsoree..."

Nyambafu! Miaka 32 Bongo bado 'laifu' haijakaa sawa. Sina kitu cha kuhonga. Nikijitahidi vocha na biere na bado pesa yangu itaniuma sana. Anayeniona mtoto yeye ana miaka 24. Halafu eti ana mahaba na baba la miaka 47. Uongo mtupu.

Sema mnavilia 'timingi' vidingi, kwa sababu wa miaka 45 kishajipanga kimaisha. Lakini nyuma yake kuna mwanamke aliyemfikisha hapo, we mdandiaji . Mnaambiwa kila kidume mwenye mafanikio nawe nyuma kuna mwanamke.

Kama una mahaba tafuta wako. Panda naye daladala za Buguruni hadi Buza. Msote hadi siku mpate gari lenu mlifaidi pamoja. Halafu akiwa na 45 kaje kapisi kali toka IFM au UDSM na kusema eti "He is caring." Uone inavyouma.

Waone kwanza. Mpaka anafikisha miaka 45 anakusubiri wewe? Miaka yote alikuwa kipofu haoni totozi au? Hizi pisi kali za kitaa na njaanuari hii zinajitoa ufahamu kabisa kama vile hakuna maisha baada ya njaa za mwezi huu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags