Watu wanadai kuwa kifo cha Tupac kilikuwa feki wakisema kuwa jamaa ilibidi afanye hivyo kwa sababu alikuwa anawindwa sana na maadui wakiwemo watu wake wa karibu pamoja na serikali ya Marekani ya wakati huo.
Miongoni mwa vitu vinavyoipa nguvu hoja hiyo ni pamoja na kitu kinachoitwa The 7 Day Theory ambayo inaelezea zaidi mahusiano ya maisha ya 2pac na namba 7.
Tupac alipigwa risasi Septemba 7, akafariki siku 7 baadaye saa 4:03 jioni. ambapo ukiangalia hesabu ya saa 4+3=7. Tupac alikuwa na miaka 25 wakati anafariki 2+5=7.!
Album yake All Eyez On Me ilitoka miezi 7 kamili kabla ya kifo chake. Na kwenye video ya I Wonder If Heaven Got a Ghetto, kuna saa inaonesha 4:03 na namba ya chumba ni 7.
Ukiachana na hiyo, 2pac Amar Shakur alikuwa ni mfuasi mkubwa wa mwanafalsafa wa kisiasa Niccolò Machiavelli ambapo ilipelekea mpaka msanii huyo kujiongezea jina la bandia na kujiita 2pac Makaveli.
Jina bandia la Tupac Makaveli lilikuja baada ya Tupac kusoma kitabu cha Niccolò Machiavelli The Prince wakati yupo gerezani akipata nafuu kutokana na jaribio la kutaka kumuua.
Alitiwa moyo sana mara baada ya kuachiliwa kutoka gerezani alibadilisha jina lake la kisanii na kuwa jina bandia linalotokana na Niccolò Machiavelli ; "Makaveli", akisema: "Kama, Machiavelli.
Machiavelli aliwahi kugushi kifo kwa miaka kadhaa alafu baadaye alirudi hadharani na alipoulizwa kwanini alifanya hivyo alijibu kuwa kuna muda inabidi ujifanye umekufa ilikufanya maadui zako wasikufuatilie.
Baadhi ya wadau wanadai kuwa rapa Tupac Shakur aligushi kifo chake baada ya kusoma kitabu cha The Prince kipindi yupo gerezani na alifanya hivyo baada ya kuona amekuwa na maadui wengi wakiwemo watu wake wa karibu na serikali ya Marekani ya wakati huo.
Upi mtazamo wako kuhusu kifo cha Tupac?
Leave a Reply