Msanii wa Bongo Fleva na mmiliki wa lebo ya muziki ya Next Level Music, Rayvanny ametolea maelezo kuhusiana na msanii wake Macvoice kuonekana akifanya shoo vijijini 'Chaka to Chaka'.
Rayvanny amesema hata yeye amekutana na video hiyo kama wengine walivyokutana nayo lakini pia mashabiki wasishangae kuona hivyo maana vitu vibaya ndio hupewa nafasi zaidi.
"Muda mwingine usichanganyikiwe kwa vitu vya mtandaoni kwasababu vitu vibaya huwa vinasambaa sana kuliko vizuri. Lakini vijana hawa ilitakiwa wasapotiwe ili wafike mbali, kama ingekuwa ni show amejaza watu wasingezungumza lakini kwakuwa kuna changamoto ndio vitu wanapenda kuongelea," amesema Rayvanny
Hata hivyo, Rayvanny amesema atatoa tamko rasmi hivi karibuni kama mkurugenzi lakini kwasasa amekutana na clip hiyo kama walivyokutana nayo watu wengine.
Utakumbuka, hii ni kufuatia video clip ambayo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii wiki hii ikimuonesha msanii wa lebo ya Next Level Music, Macvoice akipafomu kwenye show ya Chaka To Chaka ambapo mashabiki wengi wamehoji kuwa sio hadhi ya msanii wa lebo hiyo.

Leave a Reply