Rose Muhando huyu wa sasa siyo yule. Lakini thamani ya sauti yake ni ile ile. Lakini siyo yule tena. Ubora wa kutangaza neno kwa nyimbo katika mimbari kwa sasa haupo.
Mama wa watoto watatu, kwa baba tofauti. Alitengwa. Tatizo likitajwa ni matumizi ya dawa za kulevya. Na alilalamikiwa kulipwa bila kutokea katika matamasha.
Majaribu yakaja 'taimu' ambayo viongozi wa kiroho nao hawakuwa tayari tena kusaidia. Hawakutaka kumuweka chini na kumlea kiroho. Wakamuacha kondoo na dunia yake.
Neno linasema; Ni yupi mchungaji akipoteza kondoo mmoja katika mia moja awachungao, hatoacha wale tisini na tisa na kumtafuta yule mmoja aliyepotea? Hili ni neno la Mungu.
Walibaki na kondoo tisini na tisa. Rose aliachwa. Ukristo unafundisha upendo, uliomvutia Rose kutoka ile imani yake na kujiunga nao. Ule ipendo ulienda wapi kwa Rose?
Tunaambiwa samehe ukikosewa. Kosa lake ni lipi lisilosameheka? Hata kama ni kosa la kujirudia, nini maana ya samehe 7 mara 70? Pia msamaha hauna kikomo kiimani.
Wenzake walimuangalia kama sinema. Pengine ilikuwa ni nafuu kwao ya kusikika. Alisemwa kwa ubaya tu. Tuliaminishwa hawezi kurudi katika uadilifu tena.
Huyu hapa Rose Muhando. Sauti hii hapa. Na muujiza huu hapa. Mungu fundi nyie. Huumbua wanadamu kila uchwao kama hivi. Amekosa magari ila sauti ni ileile.
Leave a Reply