Albamu ya Marioo 'The God Son' imeshindikana kwenye Chart za muziki nchini. Hii ni baada ya kukaa kwa muda mrefu kama albamu namba moja inayosikilizwa zaidi.
Albamu hiyo iliyoachiwa rasmi Novemba 29, 2024, ikisheheni jumla ya ngoma 17 hadi sasa imesikilizwa zaidi ya mara 12,773,153 kupitia mtandao wa Audiomack.
The Godson imeendelea kusimama namba moja kwenye jukwa la Audiomack, ikizipindua albamu kama The Big One ya Rayvanny, Take Away The Pain ya Darassa na Peace And Money ya kwake Zuchu.
Hata hivyo, albamu hiyo imeendelea kubaki namba moja kupitia chart nyingine za muziki kama vile Apple music ambapo ilifanikiwa kuingiza trends nyimbo zaidi ya 10 kati ya nyimbo 20 kali, ndani ya wiki chache baada ya kuachiwa kwake.

Leave a Reply