Wananchi na Supu Dei

Wananchi na Supu Dei

 Yanga wana utaratibu wa mara kwa mara. Kupika supu na kulisha bure mashabiki wao pale makao makuu ya klabu. Ni tukio kubwa lenye mvuto likikusanya maelfu ya mashabiki.

Ubunifu bora wa kufanya shabiki ajione sehemu ya klabu. Inavutia sana, na kwa kiasi kikubwa supu dei imejenga bondi kati ya shabiki na klabu. Kwenye hili wamepiga bao sana uongozi wa Yanga.

Tulizoea ng'ombe zikidondoshwa kadhaa. Safari hii 'Bigi Bosi' GSM alitoa ngamia wa kilo 400. Kama kitoweo achinjwe na kuliwa supu. Shughuli hii ilikuwa siyo poa poa kwa mabingwa hawa wa nchi.

Shabiki wa Yanga jivunie jambo hili la kipekee. Uzeeni utaonesha wajukuu matukio bora ya klabu ya moyo wako. Hii ni kubwa kuliko na inajenga ukaribu wa dhati kati klabu na mashabiki wake.

Shabiki ndiye mdau namba moja wa klabu. Na supu hii ni kwa ajili ya mashabiki. Aliyetoa wazo hili akae akijua kwamba huko mbele kuna malipo. Ataishi katika mioyo na kumbukumbu ya Wananchi.

Wiki ya Wananchi ni tukio rasmi. Lipo ndani ya kalenda ya klabu. Supu dei ni mizuka tu na furaha. Huenda mbele likawa tukio rasmi la kuweka kwenye kalenda kama ilivyo Wananchi Day.

Ni utamaduni mpya kwa Yanga ya Injinia Hersi. Ni moja ya matukio yanayoipa Yanga upekee wenye upekee. Ubunifu wenye nakshi ya upendo wa viongozi kwa shabiki wa timu. Inavutia sana.

Maafisa masoko wa kampuni za kibiashara. Mnawaza nini? Yanga ni 'bigi brandi'. Tukio lolote lina 'impakti' kibiashara. Mnashindwa kushawishi mabosi kuweka pesa kwenye Supu Dei?

Hamtaki kukua kisoko, kuongeza wateja na kupanuka? Mnataka wote mkae kifuani kwenye jezi? Ndani ya saa 24, taifa liliongea Supu Dei. Mnataka ushahidi gani zaidi kujua hili tukio ni mchongo?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags