Wazo la wimbo Afande wa Dogo Paten lilipatikana hivi..

Wazo la wimbo Afande wa Dogo Paten lilipatikana hivi..

Msanii wa muziki wa singeli  Dogo Paten anayefanya vizuri kupitia wimbo wake ‘Afande’, ambao Zuchu aliomba kuufanyia remix, ameiamba Mwananchi Scoop  wazo la wimbo huo lilikuja ghafla wakati akifanya mazoezi.

"Kwanza mimi napenda kumshukuru Mungu kwa nafasi hii aliyonipa. Idea ya wimbo niliipata wakati nafanya mazoezi kwahiyo kikapatikana kitu kizuri kama hicho.

“Nikiwa nafanya mazoezi huwa nawaza kitu cha tofauti. Kwa sababu sasahivi wasanii wanaimba mapenzi sana," amesema Paten.

Amesema hakutegemea kama wimbo wake huo ungeweza kupendwa  Zuchu.

"Mimi mwenyewe sikutegemea, kuna mtu alinitumia video Zuchu akiimba wimbo wangu na akaandika ananitafuta. Sikudhani kama atafikia huko alipofikia. Mr. LG akanipigia simu akanambia nahitijika studio.

"Aise nilijisikia raha sana hata siwezi kuelezea nilikuwa na furaha sana. Nilikuwa nahisi kama utani mpaka tulipo ingia studio," amesema Paten.

Amesema yeye ni msanii mdogo kwenye gemu, lakini alioneshwa upendo mkubwa na Zuchu ambaye amemtangulia kimuziki.

“Sikutegemea kama atakuwa peace vile kanionesha upendo mkubwa. Shida tulipata kwasababu yule ni msanii mkubwa watu wengi wanamsikiliza, kwahiyo hawezi kuimba kitu chepesi. Tulikaa chini tukaumiza vichwa ili tupate kitu kizuri," amesema Paten.

Paten ameongezea kuwa tofauti na Zuchu wapo wasanii wengi ambao wamemtafuta kwa ajili ya kufanya naye kazi.

"Wapo wengi sana, kaka zangu na dada zangu walio nitangulia kwenye gemu, wananitafuta tufanye kazi kwahiyo mipango ikikaa sawa ngoma mtazisikia," amesema Paten.

Amesema singeli kwa sasa inafanya vizuri mpaka nje ya mipaka ya Tanzania hiyo ni ishara nzuri kwa muziki huo.

"Zamani Singeli watu walikuwa wanaidharau lakini manguli wameipambania mpaka imefikia hapa.  Sasa hivi inapigwa mpaka nje kwahiyo Singeli To The World," amesema Paten ambaye wimbo wake akiwa na Zuchu unatarajiwa kutoa hivi karibuni .






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags