Ceo wa Tiktok ajibu muswada wa marufuku mtandao wake Marekani

Ceo wa Tiktok ajibu muswada wa marufuku mtandao wake Marekani


Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa TikTok Shou Zi Chew amewataka watumiaji wa mtandao huo kupinga sheria ambayo inaweza kusababisha kupigwa marufuku matumizi ya TikTok nchini Marekani.

Akizungumza kwenye video aliyoiweka kwenye mtandao wa TikTok amesema endapo mtandao huo utazuiwa kuna uwezekano wa kupoteza zaidi ya ajira 300,000, kuleta athari kwa biashara ndogo ndogo milioni 7, kwa watayarishi wa maudhui na Wamarekani milioni 170 wanaotumia mtandao huo.

Ikumbukwe kuwa Machi 13, Wabunge wa Baraza la Wawakilishi nchini Marekani walipitisha muswada wa sheria wa kupiga marufuku mtandao wa TikTok nchini humo, iwapo wamiliki wake watakataa kuuza sehemu ya udhibiti wake kwa Marekani ndani ya kipindi cha miezi sita.

Hata hivyo uamuzi wa kuifunga TikTok utaiondolea Marekani mapato ya matangazo yanayokadiriwa kufikia Dola 8.66 bilioni ikilinganishwa na mapato ya Dola 1 bilioni ya mwaka 2020.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post