Chameleone Atoa Neno, Hali Yake Yazidi Kuimarika

Chameleone Atoa Neno, Hali Yake Yazidi Kuimarika


Mwanamuziki Jose Chameleone ametoa shukrani kwa mashabiki wake, marafiki, na serikali ya Uganda kwa kumuunga mkono na kuwa pamoja naye wakati akipambania afya yake.

Chameleone ametoa ujumbe huo kupitia mitandao ya kijamii baada ya kupatiwa matibabu nchini Marekani.

"Imekuwa safari ndefu, lakini upendo wenu umeshinda yote. Ninaamini na sitapoteza matumaini kwamba mkombozi wangu atanibeba daima. Utukufu kwa Mungu daima," ameandika Chameleone.

Ikumbukwe mwanamuziki huyo wa Uganda Februari 19, 2025 alifanyiwa upasuaji wa kongosho nchini Marekani katika Hospitali ya Allina Health Mercy iliyopo Coon Rapids, Minnesota.

Kwa mara ya kwanza Desemba 2024, mwanaye aitwaye Abba Marcus aliweka wazi kuwa baba yake anasumbuliwa na maradhi hayo yaliyosababishwa na uraibu wa pombe kali kwa muda mrefu.

"Natamani kila mmoja afahamu kuwa kama baba yangu ataendelea na unywaji wa pombe kwa mujibu wa madaktari hatochukua miaka zaidi ya miwili kuishi. Hii inaniumiza sana kwa sababu huyu ndiyo baba yangu niliyemfahamu kwa muda wangu wa maisha," alisema Marcus.

Baada ya taarifa hiyo ya mtoto wake, Waziri wa Nchi Vijana na Masuala ya Watoto nchini Uganda, Balaam Barugahara, alipokea agizo la Rais Yoweri Museveni la kutaka msanii huyo apelekwe Marekani kwa ajili ya matibabu.

Katika chapisho lake la hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii, Chameleone alionyesha kufurahishwa na maendeleo ya afya yake na alitoa shukrani kwa kila mtu aliyemuombea na kumuonyesha upendo.

"Nashukuru kila mtu ambaye aliniombea. Pia nilipigana sana. Shukrani za pekee kwa madaktari na wale wote ambao bila shaka waliamini kwamba kwa namna fulani nitakuwa sawa.

"Kupitia hili, nimejifunza kwamba afya na urafiki ni mambo muhimu zaidi maishani! Asante, Juliet na Julie nyinyi ni malkia na mashujaa katika hili, na kamwe msije kuacha kufanya mema kwa wengine pia," aliandika.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags