Uhusiano wa wawili hao ulithibitishwa rasmi wakati wa tuzo za BET Awards mwezi Juni, ambapo Pierre na Teyana walionekana wakiwa pamoja jukwaani, wakishikana mikono na kuonyesha mahaba yao wazi wazi mbele ya hadhira na kamera.

Taylor, ambaye ni mama wa watoto wawili, aliachana na mume wake wa zamani Iman Shumpert mwaka 2023, kwa mujibu wa tovuti mbalimbali mrembo huyo alianza ukaribu na mwigizaji huo mwezi Februari mwaka huu.
Kitendo hicho cha wawili hao kuonekana mara kwa mara kimezua mijadala katika mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya mashabiki walipokea habari hizo kwa furaha huku wengine wakimshambulia Pierre wakisema si sawa kudatishwa na mwanamke mwenye familia na mwenye umri mkubwa kwake.
Mbali na mapenzi, wawili hao pia wamekuwa wakionekana kusapoti katika kazi zao ambapo Pierre ameonekana kuhusika katika baadhi ya miradi ya kisanii ya Teyana, huku Teyana akitumia uzoefu wake kumsaidia Pierre kwenye kazi za mitindo na uigizaji.
Leave a Reply