Davido Msanii Pekee Afrika Kutajwa Orodha Ya Mfalme Charles III

Davido Msanii Pekee Afrika Kutajwa Orodha Ya Mfalme Charles III

Mkali wa Afrobeat, Davido ameripotiwa kuwa msanii pekee kutoka Afrika kutajwa katika orodha ya muziki ya Mfalme Charles III.

Akishirikiana na Apple Music, Mfalme Charles III alitangaza orodha hiyo ikipewa jina la ‘The King’s Music Room’ kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Jumuiya ya Madola ya 2025 (Common Wealth Day). Huku ngoma hizo zikipangwa kusikilizwa kwenye jukwaa hilo Jumatatu na Jumanne (Machi 10,11).

Orodha hiyo inamjumuisha msanii pekee kutoka Afrika, Davido huku wengine wakiwa ni mfalme wa reggae kutoka Jamaica Bob Marley, ikoni wa pop kutoka Australia Kylie Minogue, na mwimbaji kutoka Uingereza Raye.

Akizungumza kwenye moja ya video yake amefunguka jinsi mwingiliano wa muziki kutoka mataifa mbalimbali unavyogusa maisha yake.

“Katika maisha yangu, muziki umekuwa na maana kubwa kwangu unaleta furaha kwetu, Hivyo hii ndio hasa nilitaka kushiriki nanyi nyimbo ambazo zimeleta furaha kwangu. Asante kwa kusikiliza. Nakutakieni baraka zote zinazowezekana,” alisema

Tangu kutangazwa kwa Davido kuwa sehemu ya wasanii kwenye orodha ya nyimbo ya Mfalme, mitandao ya kijamii imejaa furaha huku mashabiki wakielezea furaha yao, wakimpongeza nyota huyo wa Afrobeat kama "30 BG" halisi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags