Moja ya jambo ambalo limeibua mijadara mingi katika mitandao ya kijamii ni kuhusiana na mwanamuziki Wizkid kuongoza (Director) mwenyewe video ya wimbo wake uitwao ‘Kese’.
Inaelezwa kuwa video hiyo ilipangwa kushutiwa Januari 16, 2025 na msanii huyo alifika eneo husika muda uliopangwa lakini muongozaji wa video hiyo (Directo K) hakufika kabisa sehemu ya kushuti, ambapo baada ya muda kupita alipiga simu na kudai kuwa hayupo vizuri kiafya.
Aidha Wizkid baada ya kupokea simu hiyo aliamua kuongoza mwenyewe video hiyo jambo ambalo lilipelekea kupokea pongezi nyingi kwa mashabiki huku wengi wao wakiwataka wasanii wengine kuiga alichokifanya Wizkid.
Ngoma hiyo ya ‘Kese’ ambayo imeachiwa siku mbili zilizopita mpaka kufikia sasa imefanikiwa kutazamwa na zaidi ya mara milioni 1.2.

Leave a Reply