Ikiwa leo ni siku ya Wapendanao ‘Valentine Day’ mwanamuziki Diamond hakutaka ipite hivi hivi ambapo ameamua kuwaziba midomo wambea kwa kutuma ujumbe wa mahaba kwa Zuchu.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Simba ameandika ujumbe mzito kwa mpenzi wake huyo ambaye pia ni msanii wake akimtaka aache kuwasikiliza wambea wa mitandaoni na aamini kuwa anampenda kweli.
“Lile neno Mtamu Kama “Nini” Ama Mzuri Kama “Nini” ama Nampenda Kama “Nini” ile “Nini” ambayo Upendo, Uzuri, Utamu na Thamani yake imepitiliza hadi Haielezeki basi ndio wewe kwangu… Wengi niliwahi kuwa nao lakini hapajatokea aliewahi kupendwa nami zaidi yako and I can not wait for our big day.
Unaniangusha tu kwa kuto kujua huyu fala Anakupenda kiasi gani na kuacha hawa Nzi wa Mitandaoni wakuendeshe kwa kutumia tuvituvitu vya kwenye kazi yangu…hawa hautakiwi kuwajibu kwa Reaction yoyote zaidi ya Kuenjoy Maisha na kufurahia Baraka tulizojaaliwa na Mwenyez Mungu - Happy Valentine Zuuh , Happy Valentine Nini,” ameandika Diamond
Utakumbuka kuwa ugomvi wa wawili hao ulianza mwezi ulioisha huku ukichochewa zaidi kuhusiana na suala zima la Zuchu kudaiwa kulazimisha kuolewa na Simba jambo ambalo lilipelekea Zuchu kutuma barua ya wazo kwa Simba kutokana na mambo anayofanyiwa na watangazaji wake ambao walikuwa wakimuumiza kiakili na kihisia.
Mbali na hilo lakini pia Zuchu alichukuwa jukumu la kuondoa utambulisho wa kuwa yeye ni msanii wa lebo ya WCB ambapo mpaka kufikia sasa hajarudisha utambulisho huo licha ya wawili hao kuonekana kuwa na maelewano mazuri kwa siku za hivi karibuni.
Aidha ukiachana na wawili hao kuwa kwenye mahusiano na kupitia migogoro kadhaa lakini wamewahi kutoa ngoma za pamoja ikiwemo Wale Wale, Mtasubiri, Raha, Cheche na nyinginezo.

Leave a Reply