


Mashabiki wengi wameinterpret hilo jina la "Zuu" kama kifupi cha "Zuchu."

Wawili hao wamekuwa wakihisiwa kuwa penzini mara baada ya kuvuja kwa video wakiwa katika gari ya Diamond na toka hapo wamekuwa wakifanya challenges na kutoa wimbo pamoja, ikiwemo 'Mtasubiri' kutoka kwenye EP ya FOA kutoka kwa Diamond.


Hata hivyo, 'Couple' hii imekuwa haiishiwi vituko vya kuzidi kuaminisha mashabiki wao kuwa wapo pamoja. Ukaribu wa kupindukia kati yao umeonekeana kukua kwa kiasi kikubwa, hadi kuonesha viashiria wazi wazi wakiwa stejini, mmmhhhh, nisiseme sana!



Kama wawili hao watakuwa ni wapenzi kweli, basi Zuchu atakuwa mwanamke sio chini ya wa 9 kutoka na msanii huyo mwenye watoto wa 4 kutoka kwa wanawake wa 3 tofauti, kutoka nchi 3 tofauti. Mambo hayo


Hakuna kati yao aliyeconfirm moja kwa moja kuwa wanadate, ingawa Zuchu ameweka hadharani kuwa anadate na mtu na wanapendana sana.,,, aaawwwww

Comment hiyo imewavuruga sana mashabiki. Tuambie, je unafikiri wawili hao wapo pamoja au la??
Leave a Reply