Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameongeza utambulisho kupitia bio yake akiandika Mrs Nasibu (Diamond Platnumz) jambo ambalo limeibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii huku kukiwa na madai kuwa wanandoa hao wapya walishaachana muda mrefu.
Mbali na hilo naye mwanamuziki Diamond ameendelea kusisitiza kuwa yeye ni mume wa mtu ambapo usiku wa kuamkia leo wakati alipokuwa akitumbuiza kwenye Mkesha wa Mwenge uliyofanyika Ilala alithibitisha hilo.
“Niwaambie kitu siku ya leo mimi sikuwa vizuri kwenye afya nilikuwa najisikia kuumwa umwa, unajua ukishakuwa ndani ya ndoa kuna kanamna yani si niwaache mambo ya Mwenge yaendelee. Mimi ni mume wa mtu jamani nyie nina kazi maalumu muda huu, hamuwezi kunielewa kwa sababu hamjaoa na kuolewa sasa ukioa ndio utanielewa,”amesema Diamond
Utakumbuka Diamond alithibitisha kufunga ndoa na Zuchu kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuchapisha picha za siku ya harusi na kushare ujumbe ambao ulizua utata katika mitandao ya kijamii ambapo aliandika.
“Miongoni Mwa vitu ambavyo nimejifunza ni Ukomavu wa kukaa kimya… Ukomavu huu unataka uvumilivu wa hali ya juu, Inataka uwe na moyo wa Subra na hasa kukaza roho pindi mtu au watu wanapokua wanakupakazia ubaya fulani kwenye jamii halaf wewe una Ukweli wake lakini unatakiwa ukae tu kimya Usijibu ilhali ukweli unao ndani.
Kwakweli si jambo jepesi linataka Ustahmilivu wa hali ya juu sana, na siwezi sema eti nauweza sana, lakini namshukuru Mwenyez Mungu amenijaalia Hekima hio kwa kiwango chake, na Nimekua nikiishi hivyo kwa Muda mrefu kukaa kimya pindi yoyote akijaribu kusema lolote zidi yangu, na ndio maana ata interview nimekua naepuka kufanya skuizi… japo si jambo jepesi lakini faida yake nimeiona na ni kubwa maana vita vyako inakua unapambaniwa na Mwenyez Mungu na inakufanya Uwe Mshindi kila siku,”aliandika Simba
Aidha aliendelea kwa kueleza “Anyways: Najua kila mmoja wenu ana picha tofauti kabisa kuhusu Diamond Platnumz na kuoa, ila tu nataka leo niwaambie kuwa huyu Diamond Platnumz alishawahi kuoa, na kuna siku nitawaambia ikawaje,”
Naye Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Walid Kawambwa wakati akizungumza na Mwananchi Jana aliweka wazi kuwa alifungisha ndoa hiyo miezi mitano iliyopita, lakini kuhusu habari za kuachana yeye hazifahamu.

“Kwanini watu wanapenda watu wengine wazini, Diamondi na Zuchu ni kweli nimewafungisha ndoa mimi toka miezi mitano iliyopita, ila hilo swali lako unaloniuliza kuhusu wameachana mimi silifahamu, sababu kama wangekuwa wameachana Diamondi angekuja kuniambia mimi.
Vile mlivyoona kwenye mitandao ni kweli ndoa wala sio kiki, ila naona watu wengi wameshtushwa na hii habari,maana mmezoea kuwasema sema Diamondi na Zuchu wazini kila kukicha sasa hili jambo la kheri lishangilieni na kuliombea kheri,”amesema Shekh Warid
Leave a Reply