Harmonize: Nakaribia kujuta kusaidiwa na Diamond

Harmonize: Nakaribia kujuta kusaidiwa na Diamond

Staa wa #BongoFleva #Harmonize ni kama ameonyesha kuchoshwa na kauli ambayo #DiamondPlatnumz anapenda kuisema mara kwa mara kuwa yeye ndiyo aliyemtoa katika muziki.

Harmonize ameyasema hayo kupitia #Instastory yake ambapo ame-post moja ya stori iliyoripotiwa na chombo cha habari cha mtandaoni nchini kikieleza namna Diamond alivyomtoa msanii huyo.

“Nilimtoa!!, nilimtoa!!, nilimtoa!!, nilimtoa!!, nilimtoa!!, nilimtoa!!, ndio ni kweli asante ila inachosha na nakaribia kujuta,”ameandika Harmonize.

Harmonize aliwahi kuwa mmoja wa zao la muziki kutoka lebo ya WCB Wasafi chini ya usimamizi wa msanii Diamond Pltanumz ambapo kwa sasa msanii huyo ametoka katika lebo hiyo na kuanzisha lebo yakree ya #KondeGang.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags