Baada ya msanii na mtayarishaji wa Bongo Fleva, Mocco Genius kumshirikisha Marioo kwenye ngoma ya Mi Nawe mwaka 2024 na kufanikiwa kufanya vizuri kwenye chart na majukwaa mbalimbali ya kusikilizia muziki wamerudi tena na ngoma ya Fitingi.
Wawili hao wamekuwa na muunganiko mzuri kila wanapokutana na kufanya kazi ya pamoja, ngoma yao ya Mi Nawe video yake imefanikiwa kutazamwa mara milioni 3 kwenye mtandao wa Youtube. Fitingi nayo inakuja kwa kasi tangu kuachiwa kwake hapo jana imetazamwa zaidi ya mara 144000 Youtube.
Lakini pia, ngoma hiyo imewagusa mashabiki wengi huku ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii hususani Tiktok ambapo ilianza kuvuma baada ya kuachiwa kwa kionjo cha wimbo huo.
Fitingi ni project ya pili kushirikiana kati ya Mocco na Marioo kama wasanii baada ya Mi Nawe lakini, Mocco amewahi kushiriki kama mtayarishaji wa muziki kwenye ngoma kadhaa za Marioo ambazo ni Pamoja na Aya iliyotoka Januari 2020 pamoja na Unanikosha ya 2020.

Leave a Reply