
Hii Ndio Hali Ya Mahusiano Ya Alikiba Kwa Sasa
Mkali wa Bongo Fleva na mmiliki wa Kings Music, Alikiba ameweka wazi hali yake ya mahusiano ya kimapenzi kwa sasa.
King ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na waandishi wa habari leo Aprili 15, 2025. Kwa kusema kwa sasa yupo mahusiano.
"Mimi nimekamilika nina mahusiano kuhusu mimi na aliyekuwa mke wangu tumemalizana kwa amani kabisa na anafuraha sana," amesema King.
Hata hivyo Kiba ameelezea kuhusu msimamo wake wa kutaka kurudi kwenye ndoa na kuelezea namna ilivyo changamoto kuipata ndoa sahihi.
"Wanasemaga ndoa mwenyezi Mungu ndio anapanga ni kweli. Hii sio tu kwa wanawake kwa sababu wanawake ndio wanaolewa, lakini pia hata kwetu sisi wanaume. Huu ni ukweli kabisa usiopingika kuna harusi na ndoa, unataka watu washangilie harusi yako sawa lakini baada ya harusi kuna ndoa.
"Lakini mwenyezi Mungu hapendi watu wakishaoana waachane kwa sababu siku ya ndoa mkishaoana mkialika watu mwenyezi Mungu na yeye huleta watu wake kwa ajili ya kuleta baraka. Sasa ikitokea mmeoana baada ya muda mkaachana mnakuwa mmesumbua watu na viumbe wa Mwenyezi Mungu.
"Ndoa sio jambo la mchezo inabidi uwe makini sana, maana kila mwanaume anaubavu wake wa kushoto na mwanamke ana ubavu wake wa kulia, utajuaje kama ni ubavu wako baada ya maisha ya ndoa kwahiyo inabidi uwe makini sana kwenye kuchagua mwenza," amesema Kiba.
Alikiba kwa sasa anajianda kufanya shoo yake ya kusherehekea miaka 20 katika muziki wa Bongo Fleva 'Decade Of Melodies'. Show hiyo inatarajia kufanyika Weekend hii Aprili 19, 2025 Kendwa Rocks visiwani Zanzibar.
Leave a Reply