Mwigizaji Carina afariki dunia

Mwigizaji Carina afariki dunia

Mwigizaji wa filamu nchini, Hawa Hussein Ibrahim (Carina), amefariki dunia leo Aprili 15,2025 akiwa nchini India alikoenda kupatiwa matibabu ya tumbo.

Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na Imelda Mtema ambaye alikuwa mtu wake wa karibu aliyekuwa akisaidia kusimamia matibabu yake.

"Ni kweli amefariki (dunia) nimepigiwa simu leo na waliopo India, hata dakika 15 hazijapita, maana jana tu nimeongea naye," amesema Imelda wakati akizungumza na Mwananchi

Hata hivyo, inaelezwa kuwa mwigizaji huyo alitarajiwa kurejea nchini leo baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa kutibu tatizo la tumbo lililokuwa likimsumbua kwa kipindi cha miaka tisa, huku akifanyiwa upasuaji wa tumbo mara 24.

Hawa aliondoka nchini Februari 24, 2025 kwenda India kupatiwa matibabu baada ya kukamilika kwa taratibu za safari na gharama ya matibabu Sh54 milioni ambazo zilitokana na michango ya serikali na tasisi mbalimbali.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags