Ishow Speed Akipata cha mtema Kuni

Ishow Speed Akipata cha mtema Kuni

Mwanamitandao na mtiririshaji wa maudhui kupitia mtandao wa YouTube Ishow Speed amejikuta akiumizwa baada ya kuingia kwenye ulingo wa mieleka wa WWE Royal Rumble 2025 na kuondolewa kikatili na wapambanaji wa jukwaa hilo

WWE Royal Rumble 2025 ilichukua hali ya tofauti baada ya MwanaYouTube huyo kuingia, lakini akaondolewa haraka na wanamieleka wa WWE Superstars 'Bron Breakker' na 'Otis'.

Mashabiki waliokuwa wakitazama tukio hilo waliachwa midomo wazi huku wakiwa na wasiwasi juu ya afya ya IShowSpeed, ambaye jina lake halisi ni Darren Watkins Jr.

IShowSpeed aliingia ulingoni kwa nambari 8, akiichukua nafasi ya Akira Tozawa ambaye hakuweza kushindana kutokana na kushambuliwa na Carmelo Hayes.

Umati ulifurahi kuona mtu wa mtandaoni kwenye ulingo huo, lakini hali ilibadilika kwa mashabiki na kuwa wasiwasi kwani IShowSpeed alivamiwa na Breakker.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags