Jason Derulo ajimilikisha Komasava mazima

Jason Derulo ajimilikisha Komasava mazima

Mwanamuziki kutoka Marekani Jason Derulo ni kama amejimilikisha ngoma aliyoshirikishwa na msanii wa Bongo Fleva Diamond iitwayo ‘Komasava’ hii ni baada ya kuonekana akitumbuiza wimbo huo zaidi ya mara moja kwenye show zake.

Derulo alitumbuiza wimbo huo usiku wa kuamkia leo Agosti 10 katika show yake iliyofanyika ‘Selman Stërmasi Stadium’ nchini Albania kwa lengo la kutoa burudani kwa mashabiki zake.

Hii inakuwa mara ya pili kwa Jason Derulo kutumbuiza ngoma hiyo, mara ya kwanza alitumbuiza usiku wa Agosti 7, 2024 nchini Kroatia kwenye show yake.

‘Komasava Remix’ ni wimbo wa Diamond aliyowashirikisha wasanii kama Jason Derulo, Khalil Harisson na Chley ambapo video yake mpaka kufikia sasa inazaidi ya watazamaji milioni 8.9 kupitia mtandao wa YouTube ikiwa na wiki mbili tu tangu kuachiwa kwake.

Aidha wimbo huo unazidi kukonga nyoyo za watu wengi kutokana na kuwepo na lugha tofauti tofauti duniani ikiwemo Kifaransa, Kichina, Kihindi na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags