Jinsi ya kufupisha link Instagram

Jinsi ya kufupisha link Instagram

Hellow guys!!! Welcome to the day of  smartphone na leo bhna nakuletea jambo muhimu sana ambalo unaweza kulifanya kwenye simu yako naona unajiuliza hapo ooohooo!! Jambo lipi hilo? Tulia this is smartphone mtu wangu.

Unajua namna ya kufupisha Link kwenye Instagram account yako? Usiowazeee sana mambo madogo hayo utaratibu mzimaa nakuekea hapa fuatilia dondoo hii ya leo.

Nafikiri kama umekua mtumiaji mzuri sana wa Instagram basi neno ‘Link kwenye Bio’ sio geni kwako neno hili maana yake basi nikwambie hapa ni ile link inayopatikana kwenye profile ya mtumiaji wa mtandao wa instagram.

Kama unavyofahamu mtandao wa instagram una uwezo wa kuweka link moja tu jambo hili limekua tatizo kwa watumiaji kubadilisha link kila mara pale wanapotaka kuwekan kitu kipya kwa watumiaji kupitia sehemu ya ‘Bio’.

Hivyo basi kuliona hilo nimekuletea dondoo ambayo itaweza kukusaidia kuweka link moja tu kwenye sehemu ya Bio lakini link hiyo itaweza kukusaidia kuelekeza watumiaji wako kwenye vyanzo tofauti tofauti.

Kwenye Bio

Kwenye bio ni moja kati ya mitandao ya kitanzania ambayo itakuwezesha kupata link nzuri ambayo inafanana kabisa na neno link kwenye bio kupitia mtandao huu utaweza kufanya vitu kadha wa kadha mfano Kuweka link za youtube, Instagram, Tik tok na mitandao mingine ya kijamii ikiwa na uwezo wa kuweka mawasiliano yako kama vile Whats up na namba za simu.

Linktree

Huu ni mtandao ambao utaweza kukusaidia sana kuweza kukusanya link zako zote na kuweka link moja, mtandao huu una uwezo wa kukupa link yenye jina lako na hivyo kukusaidia kuendeleza brand yako.

About Me

Ebwana eeeh! Huu ni mtandao mwengine pia ambao unaweza kukusaidia sana kuunganisha link zako zote kwenye link moja ,mtandao huu unakuja na domain bora sana ambayo inaweza kusaidia watu kujua zaidi kuhusu wewe au biashara yako mwanangu mweneyewe .

Seekpage

Seekpage ni mtandao mwengine ambao utakusaidia kukusanya link zako zote na kuziweka kwenye mtandao mmoja.

Kazi ni kwako mtumiaji wa smartphone nimekupa tips hizo hapo unaweza kutembea nazo na mambo yakawa mazuri kabisaa!!.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags