Mwanamuziki kutoka Canada, Justin Bieber amefunguka ukweli kuhusiana na aliyofanyiwa na rapa Diddy ambaye kwasasa yupo gerezani akisubilia kesi yake kuanza kuzikilizwa Mei 2025.
Bieber ambae amekuwa kimya tangu Diddy aanze kuhusishwa na vitendo vya unyanyasaji wa kingono amekuwa akipokea msukumo mkubwa kutoka kwa mashabiki wakimtaka afunguke yote kutokana na kuamini kuwa msanii huyo ni muhanga namba moja katika kesi za Combs.
Vyanzo mbalimbali vya habari vinaripoti kuwa Bieber ameanza kuvunja ukimya kwa watu wakaribu kuhusu yale yaliyomkuta wakati akiwa mdogo nyumbani kwa Sean Diddy Combs 'Pdiddy'
Kwa mujibu wa ‘In Touch Weekly’ wameripoti kwamba Bieber kwa sasa anakumbuka na kujadili mambo magumu aliyopitia wakati akiwa na Diddy.
"Hatimaye anavunja ukimya wake kwa marafiki zake, Jambo la mwisho ambalo Justin anataka kufanya ni kukumbuka au hata kujadili urafiki wake mgumu na Diddy" kimesema chanzo cha karibu.
Bieber hajawahi kuongea hadharani kuhusu ‘skendo’ na uvumi anaohusishwa nao kwa Diddy. Lakini amewahi kufunguka kwamba miaka ya nyuma aliwahi kuona vitu vibaya mnoo kwenye maisha yake akiwa na umri mdogo.
"Ilikuwa ngumu kwangu, kuwa mdogo na kuwa kwenye tasnia na kutojua pa kuelekea, Sitaki Mtu mwingine apitie jambo lolote nililopitia. Sitaki hilo kwa mtu yeyote." alisema Bieber wakati akifanya mahojiano na Apple music.
Bieber ambae kwasasa yupo katika majumkuma kama baba kwa mtoto wake wa kiume, Jack Blues Bieber aliyempata na mrembo Hailey, watu wake wakaribu wamekuwa wakisema huenda jamaa anapitia tatizo la afya ya akili na kama ataweka wazi maisha yake ya nyuma inaweza msaidia.
"Kama akizungumzia maisha yake ya nyuma inaweza kuwasaidia wengine, pengine atafanya hivyo. Anataka kuvunja mzunguko, mara moja na kwa wote," chanzo hicho kimeongezea.
Utakumbuka, Mabadiliko ya mtindo wa maisha kwa Bieber yalianza mara baada ya rapa Diddy kukamatwa mwaka 2024 kwa madai ya unyanyasaji wa kingono, biashara ya kingono, na biashara ya Binadamu ambapo inadaiwa kuwa Bieber ni mmoja kati ya wahanga katika matukio hayo kwani makuzi yake kimuziki tangu akiwa na umri wa miaka 15 yalikuwa karibu na Combs.

Leave a Reply