Jux Afunga Ndoa Na Priscilla

Jux Afunga Ndoa Na Priscilla

Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Jux amefunga ndoa na mpenzi wake mfanyabiashara kutoka Nigeria Priscilia leo Februari 7,2025.

Taarifa ya ndoa ya wawili hao imetolewa na baadhi ya mastaa Bongo ambao wamechapisha picha na video za harusi hiyo.

Lakini pia kupitia kurasa zao wawili hao wamechapisha picha zao zikiwaonesha wakiwa wamevalia mavazi ya harusi .

Hata hivyo ndoa hiyo imehudhuliwa na watu wachache wakiwemo ndugu wa karibu pamoja na wasanii kama vile Diamond Platnumz, Zuchu, S2kizzy, Abba, Ommy Dimpoz na wengine.


Familia ya Princila iliwasili nchini Tanzania tangu jana kwa ajili ya harusi hiyo akiwemo mama yake ambaye ni muigizaji mkubwa huko Nchini Nigeria lakini pia na ndugu zake wengine.


Mahusiano ya wawili hao yalianza mapema Agosti 2024 huku penzi lao likishamiri na kuteka mitandano ya kijamii ya ndani na nje ya Tanzania baada ya Jux kwenda ukweni nchini Nigeria.

Ikumbukwe kabla ya Jux kuwa kwenye mahusiano na Priscilla, alikuwa na Karen Bujulu. Priscilla Ajoke Ojo alionekana kwa mara ya kwanza na Jux July 19,2024 kwenye moja ya kumbi za starehe zilizopo jijini Dar es salaam. Na hii inakuwa ndoa ya kwanza kwa wapenzi hao wawili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags