Kanye Amuangukia Trump Ishu Ya Diddy

Kanye Amuangukia Trump Ishu Ya Diddy

Mwanamuziki na mfanyabiashara wa Marekani Kanye West amemuomba Rais wa nchi hiyo Donald Trump kumuachie huru mkali wa hip-hip Diddy Combs anayekabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono.

Kupitia ukurasa wake wa X ameomba msanii huyo aweze kuachiwa huru huku akiwakosoa mastaa wengine kulikalia kimya suala hili.

“Donald Trump tafadhali mwachieni huru ndugu yangu Puff wote hawa mastaa wanamwacha ndugu yetu aoze na hawasemi chochote, tulimtizama wakijaribu kumfuta Chris Brown na hakuna aliyefanya chochote,” ameandika Kanye

Mbali na hilo Ye alishiriki video ya simu akiwasiliana na mtoto wa Combs, Christian "King" Combs, akionesha mshikamano wake na familia ya msanii huyo.

Sean "Diddy" kwa sasa anashikiliwa katika gereza la Metropolitan huko Brooklyn, New York, akisubiri kesi yake ya mashtaka ya usafirishaji haramu wa binadamu na unyanyasaji wa kingono iliyopangwa kusikilizwa mahakamani kuanzia Mei 5,2025.

Mpaka kufikia sasa Diddy anakabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono takribani 15, alikamatwa kwa mara ya kwanza Septemba 16, 2024 jijini New York katika moja ya hoteli iliyopo jijini humo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags