Rapa na mfanyabiashara kutoka Marekani, Kanye West 'Ye' amewajia juu kampuni ya Adidas baada ya kutumia jina lake wakati ambao mkataba wao wa kibiashara tayari umeshamalizika.
Kanye kupitia ukurasa wake wa Instagram ameitaka kampuni hiyo kuacha kumrudisha nyuma kwani jina lake limekuwa likiendelea kujitokeza kwenye bidhaa za Adidas jambo ambalo sio sahihi.
“Unapo google Yeezy.com tovuti ya adidas inakuja mbele ya tovuti ya Yeezy, Wanachama wa adidas Acha kufanya hivi Acha kufanya harakati zako za kunirudisha nyuma Ushirikiano wetu umekamilika” ameandika Kanye
Kanye West anayejulikana kama Ye na Adidas walianza kufanyakazi pamoja Desemba 2013 walipothibitisha mkataba wa ushirikiano wa kutoa viatu vyenye jina la msanii huyo, ushirikiano wa wawili hao ulimalizika Oktoba 2022 baada ya Adidas kuvunja mkataba na rapa huyo kufuatia na maneno machafu aliyoyatoa dhidi ya Wayahudi.
Leave a Reply