Kili Paul Hana Mpinzani India

Kili Paul Hana Mpinzani India

Mashabiki na wadau wa burudani kutoka India wameonesha upendo mkubwa kwa mtengeneza maudhui maarufu Bongo, Kili Paul baada ya kutua nchini humo. hii ni baada ya Kill kuonekana kwenye moja ya filamu iitwayo Innocent inayotarajiwa kuachiwa Agosti 2025.

Kili ambaye amejizolea umaarufu kufuatia na maudhui yake yanayohusisha tamaduni za Kihindi na Kimasai aliwasili nchini humo wiki iliyokwisha kabla ya uzinduzi wa filamu hiyo uliyofanyika usiku wa kuamkia leo Mei 27, 2025.

Watayarishaji wa filamu hiyo ya Innocent iliyochezwa na nyota wakubwa kama Althaf Salim na Anarkali Marikar walitangaza ujio wa kazi hiyo katika ukumbi wa Lulu Mall, Kochi na kusema itatoka mwezi Agosti mwaka huu.

Filamu hiyo imeongozwa na Satheesh Thanvi na kutayarishwa na M. Sreeraj AKD chini ya usimamizi wa Elements of Cinema, Wakongwe wa tasnia G. Marthandan, Ajai Vasudev, Najumudeen, na Dixon Poduthas wanatumika kama wazalishaji wakuu wa filamu hiyo.

Hii sio mara ya kwanza kwa Kil kufika India hapo awali alionekana kama mgeni kwenye Bigg Boss Msimu wa 16 na pia alihudhuria hafla ya harusi ya hali ya juu nchini humo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags