Capricorn Clark ambaye alikuwa mfanyakazi wa rapa kutoka Marekani, Diddy Sean Combs ametoa ushahidi mahakamani kwa mara ya kwanza kuhusu mashtaka yanayomkabili rapa huyo.
Wakati akitoa ushahidi Clark alisema alikuwa akifanya kazi Def Jam Records kabla ya kuhamia Death Row Records ya Suge Knight. Alisema Diddy alimpeleka Central Park akiwa pamoja na Uncle Paulie ambaye alikuwa mmoja ya wafanyakazi wa karibu wa Diddy.
Clark aliendelea kueleza kazi mbalimbali alizokuwa anafanya katika shirika la Diddy, ikiwa ni pamoja na kusimamia kitengo cha wanawake kwenye kampuni ya Sean Jean, ambayo ni kampuni ya nguo.
Clark alishuhudia kuwa Diddy alimwambia kwa kuwa aliwahi kufanya kazi kwa Suge Knight, endapo chochote kitatokea, anaweza kumuua.
Clark alisema aliwahi kushuhudia Diddy akiwa na bunduki nyumbani kwake huku akizungumza kuhusu kuwa na tatizo na rapa 50 Cent.
Pia, mfanyakazi huyo wa zamani alizungumza kuhusu kutuhumiwa kuiba vito vya thamani wakati akifanya kazi kwa Diddy. Alisema alihojiwa kwa saa nyingi kuhusu hilo na Uncle Paulie na kupelekwa hadi ghorofa ya sita ya jengo ikiwa ni sehemu iliyochakaa. Anasema mlango ulikuwa umefungwa na kuna mtu alikuwa ameketi kwenye meza.
Clark alisema alifanyiwa mahojiano hayo kwa takribani siku tano na kuambiwa kama wangegundua ukweli ameiba vito hivyo wangemtupa kwenye mto. Alisema baada ya mahojiano hayo aliruhusiwa kurejea kazini na baada ya hapo wanasheria upande wa Diddy walimuuliza kwanini hakuacha kazi na kuondoka katika kampuni hiyo baada ya tukio hilo? Clark alisema "Ikiwa ningeondoka, wangefikiri niliiba."
Pia, alisema wakati anafanya kazi kwa Diddy alikuwa analala muda wa saa nne pekee kwa usiku na alikuwa analipwa dola 500000 kwa mwaka lakini hakuwahi kulipwa pesa ya muda wa ziada kazini 'Over Time'.
Aliulizwa kuhusu Diddy kuwa na makazi ya hotelini, ambapo alisema msanii huyo alipendelea maisha hayo na alichukua kamera na chupa ndogo za mafuta ya watoto na kuweka kwenye begi kila mara.
Hata hivyo jaji wa kesi hiyo, Subramanian aliendelea kujadili ushahidi uliopatikana wiki iliyopita ukihusiana na tukio la Scott Mescudi, AKA Kid Cudi akidai kuchomewa gari aina ya Porsche mwaka 2012. Ambapo waendesha mashtaka walipinga ripoti ya mpelelezi ambao unasema ushahidi wa DNA kutoka kwenye tukio hilo la kuchoma gari unaonesha muhusika alikuwa wa kike.
Utakumbuka, wiki iliyopita msaidizi mwingine wa zamani wa rapa Diddy alitoa ushahidi kuhusu tukio lililomhusisha Suge Knight, akidai Diddy alikusanya bunduki na kwenda kumtafuta wakati wa ziara yake huko Los Angeles.
Mpaka kufikia sasa zaidi ya mashahidi watano wameshatoa ushahidi dhidi ya Diddy akiwemo aliyekuwa mpenzi wa rapa huyo Cassie Ventura, Mama wa Cassie Ventura, Dr. Dawn Hughes, Gerard Gannon, Kid Cud na Clark.
Sean "Diddy" Combs alikamatwa Septemba 16, 2024 katika hoteli ya Park Hyatt, Manhattan, New York, baada ya kufunguliwa mashtaka ya shirikisho yanayohusisha njama ya kihalifu (RICO), usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono kwa nguvu, udanganyifu au kulazimisha, na kusafirisha watu kwa ajili ya biashara ya ngono.

Leave a Reply